Malachi 4

Siku Ya Bwana

1 a“Hakika siku inakuja, itawaka kama tanuru. Wote wenye kiburi na kila mtenda mabaya watakuwa mabua makavu, na siku ile inayokuja itawawasha moto,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. “Hakuna mzizi wala tawi litakalosalia kwao. 2 bBali kwenu ninyi mnaoliheshimu Jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mabawa yake. Nanyi mtatoka nje na kurukaruka kama ndama aliyeachiwa kutoka zizini. 3 cKisha ninyi mtawakanyaga waovu, nao watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu siku ile nitakayofanya mambo haya,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

4 d“Kumbukeni sheria ya mtumishi wangu Musa, amri na sheria nilizompa huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote.

5 e“Tazama, nitawapelekea nabii Ilya kabla ya kuja siku ile iliyo kuu na ya kutisha ya Bwana. 6 fAtaigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, la sivyo nitakuja na kuipiga nchi kwa laana.”
Copyright information for SwhKC